MSHAMBULIAJI wa Paris Saint Germain, Kylian Mbappe amesema bado hajafanya uamuzi wowote kuhusu mustakabali wake.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo, Fabrizio Romano, Mbappe amefanya makubaliano na Rais wa PSG kuhusu mwelekeo wake.
“Ikiwa najua ninachotaka kufanya, sipaswi kuruhusu uamuzi uendelee. Haitakuwa na maana yoyote.” Amesema Mbappe.
Wakati dunia ikitamani kufahamu mwelekeo wa Mbappe zipo taarifa zinazomhusisha kutua Real Madrid au Liverpool.
0 Comments