Miaka 3 ya ubora bila Kombe la Mapinduzi

UNGUJA, Zanzibar: LICHA ya ubora wa Yanga SC kwa takribani misimu mitatu mutawalia katika mashindano ya ndani, hata kimataifa, ajabu imekuwa ngumu kwao kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.

Mara ya mwisho kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kutwaa Kombe la Mapinduzi ni 2021 katika ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya watani zao Simba SC kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar (New Amaan complex).

Tangu hapo, wanafainali hao wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC 2023) walipita kitambo cha miaka 13 bila ubingwa huo, tangu kutwaa mwaka 2007 ikiwa ni mabingwa wa mwanzo tangu kuzinduliwa kwa michuano hiyo, walipoifunga Mtibwa Sugar.

Wababe wa michuano hiyo ni matajiri wa Chamazi, Azam FC waliotwaa mara tano (2012, 2013 kisha 2017, 2018 & 2019), wakifuatiwa na @simbascofficial waliotwaa mara nne (2008, 2011, 2015 & 2022), huku wababe kutoka Manungu-Turiani Morogoro, Mtibwa Sugar wakibeba taji hilo mara mbili (2010 & 2020).

Waliotwaa mara moja ni Miembeni ya Unguja mwaka 2009, Wana anga kutoka Kenya KCAA mwaka 2014, watoza ushuru kutoka Uganda, URA mwaka 2016 na mabingwa watetezi, Mlandege FC kutoka visiwani Unguja mwaka 2023.

Nani kutwaa Mapinduzi katika mwaka wake wa 18? Tayari Mlandege na APR rasmi watacheza nusu fainali, mtanange kupigwa Januari 10.

Nusu fainali ya pili, itaamuliwa na michezo ya leo ya robo fainali, kati ya Singida FG dhidi ya Azam FC majira ya jioni, na kipute cha usiku itashuhudiwa Jamhuri FC ya Unguja wakishindina na mnyama mkali Simba SC, zote kupigwa Uwanja wa New Amaan complex.

Fainali ya mwaka huu, inatarajiwa kuchezwa Januari 13, 2024, siku moja baada ya kilele cha miaka 60 ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments