MKATABA WA UTEKELEZAJI WA AWAMU YA PILI MRADI WA NGORONGORO LENGAI GEOPARK WASAINIWA.

Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imesaini mkataba wa makubaliano na Serikali ya China wenye lengo kuendelea na utekelezaji wa mradi wa Ngorongoro- lengai Geopark.

Mradi huo utakaogharimu Shi)ingi Bilioni 25 ambazo zinatolewa na Serikali ya China umesainiwa na Kamishina wa uhifadhi NCAA Richard Kiiza na kaimu balozi wa china Nchini Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya utalii wa Miamba ( Geopark) ambapo ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2025.

Kamishina Msaidizi mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia Urithi wa Utamaduni na Jiolojia Mhandisi Joshua Mwankunda amebainisha kuwa Ujenzi huo utahusisha miundombinu ya makumbusho kubwa na ya kisasa ya jiolojia, vyoo vya wageni katika kreta ya empakaai na kwenye nyayo za zamadamu wa kale zilizoko Laetoli.

Aidha ujenzi huo pia utahusisha sehemu za watalii kutazama na kufurahia sura za nchi (viewing platforms) katika eneo la empakaai, seneto na oldoinyo Lengai, ⁠jengo la kuwezesha utafiti na utalii wa kuona nyayo za zamadamu wa kale Laetoli, miundombinu ya kutoa tafsiri za rasilimali za utalii za kijiolojia kwenye maeneo yapatayo 100.

Kamishina Mwankunda ameeleza kuwa miundombinu hii itaongeza vivutio vya utalii na muda wa watalii kukaa ndani ye Eneo la hifadhi ya Ngorongoro pamoja na wilaya za Monduli na Karatu mkoani Arusha.

Kwa upande wake Kamishna wa Uhifadhi NCAA Bw. Richard Kiiza amepongeza jitihada za mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake zilizopelekea kupata msaada huu wa uendelezaji wa jiopaki ya Ngorongoro- Lengai kutoka nchi ya uchina.

Jiopaki Ngorongoro- Lengai ndio jiopaki pekee kwa sasa afrika kusini mwa jangwa la sahara na ya pili baraka afrika.

Utalii wa miamba na sura za nchi ni aina mpya ya utalii unaovutia wageni wengi duniani kwa sasa
.TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments