Ni Michael Fred raia wa Ivory Coast
anatajwa kubeba mikoba ya Baleke ambaye hatakuwa ndani ya kikosi cha Simba kwa
msimu wa 2023/24 kwenye mechi zilizobaki kitaifa na kimataifa.
Baleke anaondoka Simba na Moses Phiri wote
walikuwa kwenye kasi ya ufungaji wa mabao na katika Mapinduzi 2024 wote
walifunga bao mojamoja na Simba iligotea nafasi ya pili mabingwa wakiwa ni
Mlandege.
Michael kwenye ligi ya Zambia kwenye mechi
18 alizocheza alifunga jumla ya mabao 14 huku akitengeneza pasi nne za mabao.
Rekodi hizo ni balaa ikiwa zitajibu kwenye
mechi za ligi huenda akavunja rekodi ya Baleke aliyefunga mabao 8 msimu wa
2022/23 na msimu wa 2023/24 wakati anakutana na Thank You alitupia mabao 8.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na
Mawasiliano Simba alisema kuwa wanatambua uimara walionao wachezaji wao hivyo
hawana mashaka.
“Kazi kubwa ambayo ipo kwa washambuliaji
wetu wapya ni kufunga mabao tunaamini kwamba wachezaji watatimiza majukumu yao
na tutashangilia mabao,”.
0 Comments