Akizungumza na
Wananchi waliojitokeza kwa wingi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara kwa
kuwasilisha kero na Changamoto zao ikiwa ni agizo la CCM kwa RC Manyara.
ISOME NA HII >>PICHA: SENDIGA ATEKELEZA AGIZO LA MAKONDA
Mwenezi Makonda amewasihi Wataalam kutoa huduma kwa upendo kwa kutoa muda wa wananchi kujieleza.
"Niwasihi wataalam toeni huduma kwa upendo kwa wananchi hawa kwa kuwapa muda wa kujieleza na msikae kwa kuamini zaidi makaratasi kwani wakati mwengine watu hutumia nyaraka za kugushi kumdhulumu mwananchi asiye na uwezo, lazima tuelewe hilo na tutumie utaalamu wetu kuwasaidia zaidi wazee) Alisema Mwenezi Makonda.
#HABARI: Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Cuthbet Sendiga amekabidhi hundi ya shilingi milioni nne na laki tisa kwa Odilia Mkama ikiwa ni malipo yake kwa huduma ya chakula aliyokuwa anaitoa kwenye shule ya sekondari Dareda. pic.twitter.com/I2UEJ4mbTq
— Bandola Media (@bandolamediatz) January 25, 2024
Makonda ametoa rai kwa Wananchi kuwaamini Chama Cha Mapinduzi kwani pamoja na yeye kuondoka Manyara kuelekea Singida lakini bado chama kinaacha watu wake kufuatilia mwenendo mzima wa zoezi hilo na kubainisha kuwa aliwasiliana na Waziri wa TAMISEMI Ndugu. Mohammed Mchengerwa ambaye alimthibitishi watapokea taarifa zote za chama juu ya Watendaji na Watumishi wa Serikali ambao hawatafanya wajibu wao.
0 Comments