Rais Dk Mwinyi afanya mabadiliko madogo baraza la mawaziri

ZANZIBAR, Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi, leo 27 januari 2024 amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri, na kuteua viongozi, miongoni mwa uteuzi hizo ni Mudrik Ramadh Soraga, ambaye sasa ataongoza Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, akitokea nafasi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji.

Aidha, Shaaban Ali Othman amepandishwa cheo na kuwa Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, akitoka kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini. Uteuzi huo unalenga kuimarisha sekta muhimu za uchumi na uvuvi katika maendeleo ya Zanzibar.

Kwa upande mwingine,. Juma Makungu Juma ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, akibadilisha jukumu lake kutoka Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi. Hii inaonyesha azma ya serikali ya kufanya marekebisho ya kistratijia katika masuala ya fedha na mipango.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Ikulu, atakuwa Ali Suleiman Ameir (Mrembo), ambaye awali alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango. Uteuzi huu unadhihirisha dhamira ya serikali ya kuwa na uwiano mzuri wa uongozi na utawala wa nchi.

Pia, Rais Mwinyi amemteua Salha Mohamed Mwinjuma kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi.. Salha, ambaye ni Mwakilishi wa Viti Maalum kutoka Kundi la Vijana Kusini, Unguja, anatarajiwa kuleta mchango wake katika kusukuma mbele ajenda ya maendeleo ya makazi na ardhi

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments