Rais Dkt.Samia afanya uteuzi DART na TANAPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua aliyewahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Athuman Kihamia kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).

Dkt.Kihamia anachukua nafasi ya Dkt. Edwin P. Mhede ambaye uteuzi wake umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Musa Kuji kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Kuji alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

VIDEO: MSIACHE KUTUMIA OFISI ZETU KWA MSAADA WA KISHERIA

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments