RAIS MWINYI ARIDHIA SIMAI KUJIUZULU

Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi amekubali ombi la kujiuzulu la Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Mohammed Said, kuanzia leo January 26, 2024 ikiwa ni saa chache baada ya Simai kutangaza kujiuzulu nafasi yake ya Uwaziri usiku wa kuamkia leo akisema mazingira ya kutekeleza jukumu hilo yamekuwa magumu.

Simai alinukuliwa akisema “Nimeandika barua kwenda kwa Rais Dkt. Mwinyi ya kujiuzulu kuanzia leo, nimefikia uamuzi huu ambao hapa kwetu sio rahisi katika utamaduni wetu kutokana na imani yangu kwamba jukumu namba moja la Wasaidizi wa Rais wakiwemo Mawaziri ni kumsaidia kutekeleza Ilani ya Chama na inapotokea mazingira yasiyo rafiki katika kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa ustawi wa Wananchi ni vema kutafuta jawabu kwa haraka ili kazi ya kuwaletea Wananchi maendeleo iweze kuendelea na hata ikibidi kukaa pembeni”

“Mimi nimefikia uamuzi huo mgumu wa kukaa pembeni, namshukuru Rais kwa kuniteua, nitaendelea kuwa Mtiifu kwa Serikali na CCM wakati wote nitakuwa tayari kutoa ushauri wowote utakaohitajika kwa Serikali ili kuhakikisha Ilani ya Chama chetu inatekelezwa kwa uaminifu” — Simai.

#VIDEO: Wananchi Mkoani Singida Wametakiwa Kuendelea Kutoa Taarifa Kwa Jeshi La Polisi

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments