Riyad Mahrez : Tunajua maana ya AFCON

Kiungo Mshambuliaji na Nahodha wa timu ya taifa ya Algeria nyota wa zamani wa Manchester City, Riyad Mahrez anaamini kuwa kichocheo cha kushinda AFCON 2023 ni maandalizi mazuri, bahati na uzoefu.

“Nchi ambayo itakuwa imefanya maandalizi mazuri na kufurahia bahati waliyokuwa nayo, basi inaweza kwenda hadi kutwaa ubingwa,” alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32

“Uzoefu ni moja ya vitu muhimu. Mimi na wenzangu wengine waliopo katika timu ya taifa ya Algeria tunajua maana ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

“Kuanza vizuri ni silaha kubwa na muhimu. Tuliwafunga Kenya katika mchezo wetu wa ufunguzi wa Fainali za mwaka 2019 na tulishinda taji la mashindano hayo. Tulitoka sare dhidi ya Sierra Leone miaka mitatu baadae, lakini baadae tulichemsha”

Mahrez, ambaye ni mzaliwa wa Ufaransa, ambaye aliondoka katika Ligi Kuu ya England na kutua katika Ligi Kuu ya Saudia mwaka jana, alikuwa mhezaji wa kutumainiwa katika kikosi cha Algeria nchini Misri mwaka 2019.

Pia alikuwa sehemu ya kikosi kilichofanya vibaya wakati kikitetea taji lake nchini Cameroon miaka miwili iliyopita wakati kilipofungwa na Guinea ya Ikweta na Ivory Coast na kuifanya kutolewa katika hatua ya makundi.

Algeria yenye kikosi kilichochanganyika na wachezaji walioshiriki Fainali za mwaka 2019 na damu mpya, ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi ya kutwaa taji hilo katika Kundi D katika Fainali za mwaka huu ambazo zinaanza keshokutwa Jumamosi (Januari 13)

Katika Kundi lao wako na Burkina Faso pamoja na timu zilizowahi kumaliza katika nafasi ya pili, tatu na nne katika mashindano manne yaliyopita.

Timu mbili za juu katika msimamo wa kundi moja kwa moja zitakuwa zimefuzu kucheza hatua ya 16 bora na itashtua kama Algeria na Burkina Faso zitashindwa kujaza nafasi hizo mbili.

Kipa Rais MBolhi, mabeki Rarny Bensebaini na Aissa Mandi, viungo Ismael Bennacer na Sofiane Feghouli na washambuliaji Youcef Belailina Bounedjah ni wachezaji wengine waliokuwepo wakati timu hiyo ikitwaa taji mwaka 2019

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments