Roma waachana na Mourihno

                         

KLABU ya AS Roma imethibitisha kuachana na kocha Jose Mourinho kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo leo imeeleza kuwa Mourinho anaondoka jijini Roma na benchi lake la ufundi.

Mreno huyo alitua kwa Giallorossi akiwa kocha wa 60 wa klabu hiyo mwezi Mei 2021.

Mourinho aliisaidia Roma kushinda ubingwa wa Conference League huko Tirana Mei 2022 na Kombe la Europa huko Bundapest.

“Tungependa kumshukuru Jose kwa niaba yetu sote hapa Roma kwa juhudi zake tangu alipowasili klabuni hapa.” Imeeleza taarifa ya Roma.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments