PICHA: SENDIGA ATEKELEZA AGIZO LA MAKONDA

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Cuthbet Sendiga amekabidhi hundi ya shilingi milioni nne na laki tisa kwa Odilia Mkama ikiwa ni malipo yake kwa huduma ya chakula aliyokuwa anaitoa kwenye shule ya sekondari Dareda.

Zoezi hilo limefanyika asubuhi ya leo mara baada ya jana Mama huyo kumuomba usaidizi Katibu wa NEC itikadi,uenezi na mafunzo wa CCM Paul Makonda anayeendelea na ziara yake mkoani Manyara.

Katika hatua nyingine Makonda amefungua rasmi kliniki ya kuwasikiliza wananchi wa Manyara wanaokabiliwa na kero na changamoto mbalimbali zoezi linaloongozwa na Mkuu wa mkoa na wakuu wa idara mbalimbali.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments