SERIKALI KUJENGA MINARA YA MAWASILIANO ENEO LILILOATHIRIKA NA MAFURIKO HANANG

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye (Mb) ametembelea na kuona sehemu zilizoathiriwa na maporomoko ya matope Wilayani Hanang, kukagua Miundombinu ya Anuani za Makazi na Posta pamoja na Kuongeo na Waandishi wa habari.

Akiwa katika ziara hiyo Waziri Nape amevishukuru na kuvipongeza vyombo vya habari kwa kazi kubwa ya kuhabarisha umma kipindi chote ambacho wilaya ya hanang ilikumbwa na Janga kubwa la maafa.

Katika hatua nyingine Mhe. Nape amesema serikali imeandaa minara zaidi ya 30 ambayo itasaidia kupunguza changamoto ya mawasiliano katika kata ya Gendabi na maeneo mengine ya Mkoa wa Manyara.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amemshukuru Mhe. Nape kwa kusudio lake la kuhakikisha mawasiliano ya Simu kwenye maeneo ya vijijini katika Mkoa wa Manyara yanaimarishwa.
#VIDEO: Wananchi Mkoani Singida Wametakiwa Kuendelea Kutoa Taarifa Kwa Jeshi La Polisi

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments