DAR ES SALAAM: Mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake kati ya JKT Queens na Simba Queens uliokuwa upigwe leo Januari 09, 2024 umeshindwa kufanyika baada ya timu hizo kupishana uwanja wa kuchezea.
Kupitia taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii, ilielekeza mchezo huo ungechezwa Uwanja wa Azam Complex.
Simba Queens waliwasili uwanjani hapo kama ilivyoelekeza taarifa ya shirikisho lakini JKT Queens wao wakatia timu katika uwanja wao wa nyumbani wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni jijini Dar es Salaam.
Awali, Afisa habari wa JKT Queens, Masau Bwire alisema wanaamini mchezo huo utachezwa katika uwanja wao wa nyumbani
“ Tunaamini Mchezo kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizopo hasa mwenyeji kutumia uwanja wake wa nyumbani wapinzani wetu watakuwa hapa kwaajili ya mchezo huo, niwaalike Watanzania wote kuja kuangalia mchezo huo.
Baada ya sinema hiyo wasimamizi wa mchezo huo waliamua kuhairisha mchezo huo huku taarifa zaidi zikisubiriwa.
0 Comments