Singida Wajivunia Kijiji Cha Nyuki Kuendelea Kufuga Nyuki Kibiashara

           

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. FATUMA MGANGA ameipongeza Kampuni ya Kijiji cha Nyuki kwa kuendelea kuwekeza katika masuala ya Ufugaji Nyuki kibiashara hali iliyosababisha kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na mdudu Nyuki hapa nchini.

                    

Dkt. Mganga alisema hayo wakati akizungumza na watu wenye Ulemavu wa Kusikia, ambao wamekuja kupata mafunzo ya Ufugaji Nyuki kibiashara katika Kijiji cha Nyuki.

Alisema kupitia Kijiji cha Nyuki Watu wengi waendelea kupata fursa ya kufuga Nyuki kibiashara na soko la kuuza Asali yao Kijiji cha Nyuki.

Aidha Dkt. FATUMA MGANGA alisema Mkoa wa Singida utaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji ili kuvutia wawekezaji wengi katika mkoa huo.

Aliongeza kuwa mkoa wa Singida unawakaribisha watu na Taasisi mbalimbali zenye nia ya kuja kuwekeza mkoani Singida kutokana mazingira mazuri yaliopo katika mkoa wa Singida.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kijiji cha Nyuki PHILEMON KIEMI aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuwaunga mkono Wawekezaji waliopo katika mkoa wa Singida ili waendelee kutoa ajira kwa vijana wengi.

KIEMI alisema pia Kijiji cha Nyuki kitaendelea kutoa mafunzo kwa wananchi wa Mkoa wa Singida na Mikoa mingine juu Ufugaji wa Nyuki kibiashara ili kuongeza watu watakaowekeza kwenye Sekta ya Nyuki.

Alisema mpaka sasa zaidi ya Watu 700 wa Mkoa wa Singida wamepata mafunzo ya Ufugaji Nyuki kibiashara, na kugawa mzinga mmoja na vifaa vingine vya ufugaji nyuki kwa kila mshiriki wa mafunzo hayo.

Hata hivyo ametoa wito kwa Wananchi, Makampuni na Taasisi kuja kujifunza namna ya kufuga Nyuki kibiashara ili kuongezea uzalishaji wa mazao yatokanayo na mdudu Nyuki.

Nao baadhi ya wanafunzi Wenye Ulemavu wa Kusikia wameishukuru Kampuni ya Kijiji cha Nyuki kwa kutoa mafunzo hayo na wameahidi kwenda kusambaza Elimu waliopata kwa Jamii.

Walisema kupitia mafunzo hayo sasa wataenda kuanzisha vikundi vya ufugaji nyuki ili waweze kuongeza vipato vyao na familia zao.

Jumla ya wanafunzi 50 Wenye Ulemavu wa Kusikia wametoka katika mikoa yote ya Tanzania kuja kujifunza ufugaji Nyuki kibiashara katika Kijiji cha Nyuki kilichopo Kisaki Mkoani Singida.

#VIDEO: Wananchi Mkoani Singida Wametakiwa Kuendelea Kutoa Taarifa Kwa Jeshi La Polisi

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments