RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema shirikisho hilo haliungi mkono kauli ya kocha Adel Amrouche kwamba Morocco inapanga muda na waamuzi wa michezo yao.
“Sisi kauli yetu tunayoitoa tuko mbali na kauli zake na hatuzikubali, na tunajua tutafanya nini tuko kwenye mashindano, kuchukua hatua ambazo tutaona tunastahili kuchukua.” amesema Karia.
Mapema leo akiwa nchini Ivory Coast wakati akizungumza na waandishi wa habari, kocha huyo alisema Morocco inapanga ratiba za mechi zao na waamuzi pia.
Karia amesema shirikisho litaongea na kocha huyo kudhibiti kauli zake ili kuepuka changamoto zingine zinazoweka kuwakuta.
0 Comments