Usafiri wa treni mikoani wasitishwa

DAR ES SALAAM:SHIRIKA la Reli (TRC) limesitisha huduma za usafiri wa treni, kutoka Dar es Salaam kuelekea katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Katibu, Kigoma, Shinyanga na Mwanza pamoja na mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Taarifa iliyotolewa leo Januari 18, 2024 na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa TRC, Jamila Mbarouk imeeleza sababu za kusitisha huduma hiyo ni kutokana na uharibifu wa miundombinu ya reli uliotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

“Wahandisi wanaendelea na matengenezo katika maeneo yaliyoathirwa na mvua.” Imeeleza taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa huduma hiyo inatarajiwa kurejea Januari 23 2024 baada ya kukamilika kwa matengenezo hayo.

SITAWAVUMILIA VIONGOZI WANAOSHINDWA KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO ASEMA PETER SERUKAMBA

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments