#VIDEO: Wakurugenzi Msiwatumie Maafisa Kilimo Kukusanya Ushuru wa Halmashauri - PAUL MAKONDA

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi - CCM Taifa, PAUL MAKONDA amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuacha kuwatumia Maafisa Kilimo kama Wakusanya Ushuru wa Halmashauri na badala yake wafanye kazi zao za kuwasimamia wakulima ili waweze kuzalisha kwa tija.

Makonda alitoa agizo hilo Mkoani Singida, katika kijiji cha Sagara Wilaya ya Singida, wakati akitokea mkoani Manyara akiwa katika Ziara yake ya kuimarisha Chama na kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Alisema Serikali imetoa fedha nyingi na Vifaa kwa ajili ya Maafisa Kilimo ili waweze kuwatembelea wakulima kuwapa ushauri juu ya kilimo bora, lakini baadhi ya Wakurugenzi wamekuwa changamoto kwa kuwatumia Maafisa Kilimo hao kama wakusanya ushuru.

Aidha alisema Chama hakitawavumilia wakurugenzi na viongozi ambao wanakwamisha juhudi za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan za kuinua Sekta ya Kilimo.

Hata hivyo pia alimuagiza Waziri wa Kilimo Hussen Bashe kuhakikisha anawachukia hutua maafisa Kilimo ambao wanashindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Alisema akishindwa kuwachukulia hatua, Chama kitachukua hatua juu yake na kwa watendaji hao.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Sagara Wilaya ya Singida waliasema wanakabiliwa na changamoto ya ubovu wa baadhi ya Barabara ambazo ni muhimu kwa shughuli mbalimbali za kijamii.

Walisema ubovu wa Barabara hizo imekuwa ni changamoto kubwa kwa akina Mama hasa wakati wa kufuata huduma mbalimbali ikiwemo huduma za Afya.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments