Naibu SILINDE ametoa taarifa hiyo wakati akizundua zoezi la Usambazaji wa Mbegu Bora za Alizeti zenye Ruzuku kwa wakulima wa Mkoa wa Singida ambapo Mkoa wa Singida kwa msimu huu utapokea Tani 600 za Mbegu.
Amesema tangu Wiraza ianza utaratibu wa kusambaza Mbegu Bora za Alizeti Uzalishaji umeongezeka hivyo akaziagiza Halmashauri kutoa ushirikiano kwa Wizara na Wakala wa Mbegu ili zoezi la usambazaji wa Mbegu Bora za Alizeti liweze kufanikiwa kwa kuwafikia wakulima wote.
Pamoja na kuwataka wakuu wa Wilaya kwenda kusimamia suala la usambazaji wa Mbegu amewataka Viongozi kwenda kusimamia makubaliano ya Serikali ya Mkoa ya kuanzisha Mfumo wa Stakabadhi Ghalani kwa lengo la kuwasaidia wakulima kuuza mazao yao kwa bei halali.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba alitoa maelekezo kwa Wakulima kutumia Mbolea kwenye mashamba yao ili waongeze Uzalishaji.
KUTOKA SINGIDA
0 Comments