Zuchu akubali ombi la Anjella kufanya kolabo na yeye

Hatimaye msanii Zuchu amemjibu mrembo mwenzake katika tasnia ya Bongo Fleva, Anjella kuhusu ombi lake la kutaka kufanya kolabo na yeye.

Hii ni baada ya Anjella kudai kwamba ndoto yake ya muda mrefu imekuwa kufanya kolabo na Zuchu lakini pia akafichua kwamba juzi kati walikutana lakini akaogopa kumwambai suala kama hilo.

“Natamani sana kufanya kolabo na Zuchu, ila juzi nimekutana naye kwenye studio Fulani lakini sikuweza kumwambia hili suala, nitafurahi sana hili likija kutokea,” Anjella alisema.

Baadaye hili ungamo lilimfikia Zuchu ambaye kupitia instastory yake alijibu akionekana kukubali kufanya kolabo hiyo ili kutimiza ndoto ya muda mrefu ya malkia mwenzake.

Zuchu aimtaka Anjella kutuma wimbo ili ausikize na kujua ni wapi ataongeza mishororo yake katika harakati nzima ya kutengeneza ngoma ya kikoa.

“Tuma wimbo dadangu, hebu na tuifanye,” Zuchu aliandika akimtag Anjella.

Kwa muda mrefu, wengi wamekuwa wakifikiria kwamba wawili hao hawako katika hali nzuri ya maelewano kutokana na hali ambayo walijikuta.

Itakumbukwa Anjella alikuwepo kama mmoja wa wasanii waliokuwa chini ya lebo ya Konde Music Worldwide inayomiliiwa na Harmonize wakati huo huo Zuchu yuko chini ya WCB Wasafi inayomilikiwa na Diamond Platnumz.

Kutokana na Diamond na Harmonize kutokuwa na ushirikiano mwema kwenye tasnia ya muziki, baso moja kwa moja mashabiki wengi walikuwa wakijua kwamba mtu yeyote ambaye yuko kwenye lebo ya WCB Wasafi moja kwa moja anakuwa adui kwa yule aliyeko Konde Gang pasi na kujali kiini cha ugomvi wa wamiliki wa lebo hizo.

Lakini baada ya Anjella kutoka mwaka juzi, inaonekana amepata uhuru kabisa wa kujiamulia kile ambacho anakitaka, na kuweka wazi kwamba anataka kolabo na Zuchu ni moja ya uamuzi wake wa kujizungumzia pasi na vikwazo akiwa kama msanii huru.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments