DAR ES SALAAM; Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko amewataka wasanii nchini kulipa Taifa heshima kwa kuzingatia lugha, utamaduni na mila za Tanzania.
Akizungumza kwenye mkutano wa wa wadau wa Utamaduni jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wasanii na wadhamini, Dk Biteko amesema hilo likifanyika litasaidia kulipa Taifa heshima.
“Sanaa ina wenyewe, nimeona jambo kwamba mmekataa kupuuza utamaduni wa taifa letu na mmeamua kwa pamoja kuupa heshima utamaduni wetu,” amesema Dk Biteko.
Naye Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro amesema serikali ina mikakati mikubwa ya uendelezaji wasanii nchini.
0 Comments