Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida haijaridhishwa na kasi ya Ujenzi wa Mradi wa Skimu ya Umwagiliaji ya Msingi wilayani Mkalama, na imemtaka Mkandarasi wa Skimu hiyo kuongeza kasi ili ikamilike kwa wakati.
Kamati hiyo ya Siasa haijaridhishwa baada ya kutembelea kukagua Skimu hiyo ikiwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Singida.
Walisema ni Miezi 8 sasa imepita toka eneo hilo likabidhiwa kwa mkandarasi wa kujenga Skimu ya Umwagiliaji ya Msingi na kazi ya ujenzi ikiwa ni 10% tu ya utekelezaji wake kwa kipindi cha miezi hiyo 8.
Aidha walimtaka mkandarasi huyo kuhakikisha anamaliza Mradi huo kwa wakati ili wananchi waanze kufanya shughuli za kilimo.
Hata hivyo Kamati hiyo ya Siasa Mkoa wa Singida iliishukuru Serikali kwa kutoa Bilioni 34 kwa ajili ya Ujenzi wa Skimu ya umwagiliaji Kata ya Msingi wilayani Mkalama.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Singida MARTHA MLATA alisisitiza kuwa Mradi huo ni lazima ukamilike kwa wakati ili wananchi waweze kuzalisha mazao mbalimbali.
Aidha MLATA aliwataka TANESCO kupeleka miundombinu ya Umeme katika eneo hilo ili kama kuna wawekezaji wa Viwanda wasipate changamoto ya kukosekana kwa umeme.
Hata hivyo pia alimtaka Wakala wa Barabara za Vijijini na Njini - TARURA kuhakikisha miundombinu ya Barabara inakuwa mizuri kwa ajili ya shuguli za usafirishaji wa Mazao.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Msingi nao waliishuru serikali kwa kutoa Fedha za kujenga Mradi huo ambao utawasaidia kilima mara mbili kwa mwaka.
Walisema kupitia Mradi huo, wataumia uchumi wao na taifa kwa ujumla na hata kuongeza mapato ya Halmashauri yao.
0 Comments