MAMIA WAJITOKEZA KUMUOAGA LOWASA KARIMJEE, WAKO PIA VIONGOZI WA DINI

MAMIA ya watu wamejitokeza katika Viwanja vya Karimejee jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, huku zoezi hilo likitarajiwa kuongozwa na Makamu wa Rais, Dkt. Phillip Mpango.

Leo Jumanne, Februari 12, 2024, mwili wa Lowassa unatarajiwa kuagwa katika Viwanja hivyo ambapo viongozi mbalimbali wa kiserikali akiwemo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mawaziri wengine wamehudhuria.

Mbali na mawaziri wa Tanzania Bara, Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Othman Masoud Othman na mawaziri kadhaa wa visiwa hivyo, wamehudhuria kwa ajili ya kushiriki hafla hiyo ya mwisho kwa Lowasa.

Viongozi wengine wa vyama vya siasa akiwemo Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na viongozi wa dini, wamehudhuria shughuli hiyo

Jeneza lililobeba mwili wa Lowassa huku likiwa limefunikwa na bendera ya Tanzania, limeingia uwanjani hapo majira ya 10.20.

Shughuli hiyo inatanguliwa na ibada fupi inayoongozwa na Mchungaji Joseph Mlaki, wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Azania Front.

Lowassa anatarajiwa kuzikwa kijijini kwao Monduli jijini Arusha, Jumamosi ya Februari 17 mwaka huu.
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments