YANGA imetangaza kuwa mechi yao ya kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad itakuwa siku ya kiungo Pacome Zouzoua PacomeDay‘ Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo. Ali Kamwe amesema.
Ali Kamwe amesema kuwa mtoko wa siku hiyo ni mwendo ‘bleach’ iwe kichwani ama kwenye kidevu.
“Uongozi na benchi la ufundi tumekubaliana kama taasisi Jumamosi ikawe Pacome Day, ukisema Pacome Day mwisho unamalizia Kitaalamu zaidi, unaweza kupaka rangi kichwani au kwenye ndevu. Kama huwezi kupaka rangi basi unaweza kujichora chochote na wanawake wanaweza kupaka kucha rangi.”amesema Ali Kamwe.
Yanga itashuka dimbani Jumamosi hii katika mchezo wa ligi hiyo uwanja wa Mkapa kutafuta nafasi ya kucheza robo
0 Comments