NEWS ALERT : RAIS WA NAMIBIA AFARIKI DUNIA


HAGE Geingob Rais wa Taifa la Namibia amefariki dunia akiwa na miaka 82 kutokana na maradhi ya saratani yaliyokuwa yanamsumbua.

Kwa mujibu wa shirika la Utangazaji la Al-Jazeera imeripotiwa kuwa Hage amefariki dunia leo jumapili katika hospitali ya Lady Pohamba akiwa amezungukwa na mke pamoja na watoto. 

Aidha makamu wa Rais wa Taifa hilo Nangolo Mbumba ametoa taarifa ya kifo hicho kupitia ukurasa rasmi wa mtandao wa kijamii wa Facebook wa Hage Geingob na kuwataka raia wa nchi hiyo kutulia wakati Serikali ikifanya taratibu za mazishi.

Mwezi uliopita Ofisi ya Geingob ilitangaza kuwa kiongozi huyo ameanza matibabu ya saratani ambayo haikuelezwa kwa undani zaidi.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments