Rais Samia kuanzisha chuo masomo kidijitali

 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kuanzisha chuo maalum kitakachojumuisha vijana kusoma kidijitali ambapo ujenzi wake utaanza katika mwaka wa fedha 2024/2025

Majaliwa amesema hayo leo, Februari 15,2023 jijini Dar es salaam kwenye mkutano wa ‘Future Ready Summit’ ulioandaliwa na Kampuni ya Mawasaliano ya Vodacom ambapo Waziri Mkuu ameipongeza kampuni hiyo kwa kuwa na maono ya kuwekeza kwa jamii na kuwawezesha wasichana kwa kuwapatia mafunzo ya kidijitali kupitia programu ya ‘code like a girl’.

Aidha, Majaliwa ametoa wito kwa viongozi wote wa Serikali, sekta binafsi, wadau wa maendeleo na wananchi kwa ujumla kuweka mikakati ya pamoja kukuza ushirikiano na kuwekeza katika miundombinu ya Tehama na kuwekeza katika ujumuishi na udijitali wa kifedha.

Aidha, ameyataka makampuni mengine kuiga mfano kwa Vodacom kwa kuandaa programu ya ‘code like a girl’ jambo linalowasaidia wanawake kuwa na ufanisi kidijitali kwenye dunia ya sasa na kupunguza uhaba wa ajira huku wakiendana na kasi ya teknolojia.

Awali, akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape  Nnauye amewatoa hofu Watanzania katika mapinduzi haya ya teknolojia akisema kumekuwa na mapinduzi ya kiteknolojia ya kidunia ambopo moja ya hofu kubwa ya watu wanachoogopa ni kupoteza kazi hivyo amewatoa hofu kuhusu kukukua kwa kasi ya kiteknolojia .

“Kumekuwa na mjadala wa mapinduzi ya Teknolojia yanayoedelea…. lakini hofu imetanda kwamba kunakuwa na hatari ya watu kupoteza kazi….. Nitumie fursa hii kuwatoa hofu Watanzania, mapinduzi haya hayakwepeki lazima tutakwenda na ni kazi yetu kujipanga, tujipange kwa kujadiliana, kuwekaza, kuweka ujuzi na sisi kusonga mbele kwasababu dunia inakwenda huko nasisi inabidi twende”. Nnauye amesema.

Nnauye ameongeza kwa kusema kuwa kama wizara moja ya kazi ya wizara hiyo ni kutengeneza sheria ambazo zitawezesha ukuaji wa teknolojia, na kumuhukikishia Waziri Mkuu kuwa Tanzania ipo tayari kwenda mbele kwenye mapinduzi hayana mapinduzi ya tatu ya viwanda.

Programu hiyo inayosimamiwa na Vodacom ijulikanayo kama “code like a girl” ilianzishwa mwaka 2018 na inajumuisha wasichana 70 wenye umri kati ya miaka 14 hadi 19.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments