Serikali, PPP kushirikiana ujenzi wa barabara

WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema Serikali imepanga kuanza ujenzi wa barabara kwa ushirikiano wa Sekta Binafsi na Umma (PPP) ili kuharakisha ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali nchini.

Bashungwa ametoa kauli hiyo leo bungeni jijini Dodoma alipowasilisha majibu ya wizara hiyo kuhusu taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu.

“Tutajenga miundombinu ya barabara kwa kushirikiana na wabia katika mfumo wa PPP, hii itaisaidia serikali kuhakikisha inakuwa na miundombinu bora, na kwa sasa tunaanza na barabara ya Dar es Salaam -Dodoma ambayo itakuwa ni barabara ya ‘Express Way’ ujenzi wa barabara hii utasaidia pia kupunguza foleni”. amesema Bashungwa.

Bashungwa amesema aliunda kamati ya kuchambua mapungufu yaliyopo kwa wakandarasa wazawa ikiwa ni pamoja na mitaji, mitambo, uwezo wa kusimamia miradi ambapo kamati hiyo imeshakamilisha taarifa ya awali ambayo itawasilishwa katika bunge kwa ajili ya kujadiliwa.

Bashungwa amewaondoa wasiwasi wabunge juu ya utekelezaji wa miradi ya EPC+F ambapo amesema wakandarasi saba wanaotekeleza miradi hiyo wanafanya mapitio upembuzi yakinifu uliofanywa na Wakala wa Barabara (TANROADS) mwaka 2017 ili kupata taarifa halisi za ujezi wa barabara hizo na ukikamilika miradii itaanza.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments