SERIKALI YATOA BIL. 1.3/- KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA ELIMU MANISPAA YA SINGIDA.

Serikali imetoa Shilingi Bilioni Moja Nukta Tatu (1.3) kwa Manispaa ya Singida kwa ajili ya kutatua changamoto ya Madarasa na Matundu ya Vyoo katika baadhi ya shule zenye Uhaba wa Madarasa na Vyoo.

Meya wa Manispaa ya Singida YAGI KIARATU alisema hayo katika Kikao cha Baraza la Madiwani la Manispaa hiyo cha kujadili Taarifa za maendeleo kwa kila Kata.

Alisema wao kama Halmashauri wataendelea kutafuta usaidizi nje ya Bajeti zao kwa Wadau wa maendeleo ili kusaidia kutatua changamoto zingine ikiwemo uhaba wa Madawati, ili kuondoa kero ya wanafunzi Kukaa chini 

Aidha KIARATU aliwataka Madiwani kusimama Miradi yote iliyopo katika maeneo yao kwa kuwashirikisha Wananchi na ikamilike kwenye Ubora unaotakiwa.

KIARATU pia amewataka Madiwani kutatua changamoto zinazowakabili wananchi ili kuondoa malalamiko ya wananchi pindi viongozi wakubwa wanapokuja.

Kwa upande wao Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida waliishukuru Serikali inayoongozwa na Rais SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuendelea kutoa fedha nyingi katika Kata zao kwa ajili ya kutekeleza Miradi mbalimbali ya maendeleo ili wananchi waweze kupata huduma karibu na makazi yao.

Walisema kuwa serikali imetoa fedha nyingi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Singida na Miradi mingi imetekelezwa na kutatua changamoto nyingi zinazoikabili Wananchi.

Pamoja na kuishukuru Serikali, lakini pia walisema bado kuna changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wananchi ikiwemo ubovu wa miundombinu ya Barabara.

Walisema Barabara ni kiunganishi kizuri cha mawasiliano lakini kuna baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Singida kuna ubovu wa Barabara hali inayosababisha wananchi kukosa huduma muhimu za kijamii.

Hata hivyo wameiomba serikali kuhakikisha inaendelea kumalizia Miradi ambayo inaendelea kutekelezwa, hasa Miradi ya Afya, Elimu na Miundombinu ya Barabara. 

Katika Kikao hicho, Katibu wa CCM Wilaya ya Singida Mjini NEEMA LUNGA alisema Chama kinaridhishwa na utendaji wa Madiwani wa Manispaa ya Singida katika kusimamia Miradi na fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya Maendeleo.

LUNGA pia alitoa wito kwa Madiwani kuhakikisha wanasimamia Miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao inakamilika kwa wakati ili Wananchi waanze kupata Huduma.

Aidha alisema ni lazima Madiwani weende kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo yao kueleza mazuri yaliyofanywa na serikali ya Rais SAMIA SULUHU HASSAN na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
MAAZIMIO BUNGE KUHUSU VIWANJA:

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments