Sh trilioni 1 kuboresha elimu nchini

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka miwili imetumia Sh  trilioni 1.29 kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Amesema kati ya fedha hizo Sh bilioni 454.3 zimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule za elimu ya awali na msingi ambapo jumla ya shule mpya zilizojengwa ni 342, vyumba vya madarasa 9,189, nyumba za walimu 346, mabweni 28 na ukarabati wa shule kongwe 45.

Amesema hayo  Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Taarifa kuhusu utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo 2014, Toleo la 2023 na Mitaala ya Elimu ngazi ya Elimu Awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

Amesema utekelezaji wa mtaala mpya umeanza katika ngazi ya Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi – Darasa la I na III, Elimu ya Sekondari Kidato cha Kwanza katika baadhi ya fani za amali katika shule 96 za Serikali na Binafsi ambazo zina miundombinu wezeshi kama karakana na walimu wa fani hizo.

Majaliwa amesema Sh Bilioni 837.8 zimetolewa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo zimetumika katika ujenzi wa shule za Sekondari mpya 486, vyumba vya madarasa 21,990, nyumba za walimu 280, mabweni 221, ukarabati wa shule kongwe 21, maabara 151 na mabwalo 23.

Aidha, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kumshukuru na kumpongeza  Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha hizo zilizoboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia shuleni ambazo zimeongeza udahili wa wanafunzi wa elimu ya awali msingi na sekondari pamoja na kuimarika kwa ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments