Taasisi ya Mandela yaiomba Serikali mazingira safi ufundishaji

Makamu Mkuu wa Mipango,Fedha na Utawala ,Profesa Suzanna Augustino kutoka Taasisi ya Sayansi ya Tenknolojia ya Nelson Mandela aimeiomba serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayosaidia watoto wa kike na wasichana kupenda masomo ya sayansi ili taifa liweze kuwa na wataalam wabobezi katika fani ya sayansi na nyuklia nchini.

Profesa Suzanna alitoa rai hiyo Jana wakati wa kusherekea siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi iliyofanyika jijini Arusha na kukutanisha wanafunzi wa shule mbalimbimbali na wada wa masomo ya sayansi

Alisema endapo shule nyingine za masomo ya sayansi zikiendelea kujengwa sanjari na walimu wakitumia mbinu bora za ufunzaji wanafunzi wanaosoma masomo hayo ya hesabu,fikizika,bailojia na ubunifu wataweza kuwa wataalam wabobezi katika fani za sayansi na kuleta tija zaidi kwa taifa .

“Tunapofundisha wanafunzi madarasani lazima tuwape mafunzo kwa vitendo ili wapende somo husika naamini ujenzi wa shule za sekondari za wasichana na zilizopo sasa utazalisha vipaji vingi kutoka kwa wasichana na wanawake na kamwe msiogope mkahisi kuwa hamuwezi hapata kila mtu anaweza kutimiza malengo’

Pia alitoa rai kwa viongozi mbalimbimbali wa Kata na serikali wanapotaka kuanzisha shule washirikishe wananchi ili wachague maeneo husika ya ujenzi wa shule kwania ya kuwaondolea vikwazo wanafunzi wakike wanapoend shuleni kusoma na wanaporudi majumbani.

Naye ProfesaNuhu Hatibu ambaye ni mwekezaji binafsi katika masuala ya elimu na ubunifu kutoka shule ya Arusha Science ilipongeza serikali kwa kuja na sera mpya ya elimu ambayo ni ya kwanza kwa nchi za Afrika na Tanzania inayoleta chachu ya kuingiza masuala ya sayansi na bunifu ikiwemo watoto wakike na kiume kutengeneza mazingira rafiki lakini pia serikali iangalie namna bora ya kuwezesha mwanafunzi akimaliza shule aweze kupata ajira moja kwa moja serikalini badala ya kumwacha akose ajira

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments