SHIRIKA la Umeme (TANESCO) limesema kukatika kwa umeme katika baadhi ya maeneo jioni ya leo kumesababishwa na hitilafu katika Gridi ya Taifa.
Taarifa iliyotolewa jioni hii na Kurugenzi ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma TANESCO imeeleza kuwa juhudi za kurejesha huduma hiyo katika maeneo yaliyoarithika zinaendea.
Shirika hilo limewataka wateja wake kuendelea kuwa watulivu wakati jitihada zikiendelea.
0 Comments