Tanzania kufuata nyao za Japan uendeshaji michezo

MKURUGENZI Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema wana mpango wa kutumia Bahati Nasibu ya Taifa katika kukuza pato la kuendesha shughuli za michezo nchini kama wanavyofanya chama cha soka cha nchini Japan

Msigwa amesema njia hiyo wamejifunza kutoka Japan walipofanya ziara hivi karibuni na kujionea namna inavyotumia Bahati Nasibu ya Taifa lao kujiingizia fedha nyingi zinazosaidia kunyanyua michezo.

Msigwa amesema Japan inaingiza Sh bilioni 300 kupitia Bahati Nasibu ya Taifa wakati Tanzania Sh bilioni 35 ndiyo bajeti ya wizara hivyo kuna cha kujifunza kupitia mipango inayowafanya kunyanua sekta yao ya michezo.

“Nchini Japan tumejifunza mengi lakini kubwa mchezo wa kubahatisha kwa kutumia Bahati Nasibu ya Taifa inawaingizia Sh bilioni 3000 kwa mwaka nasi tumeona fursa hiyo tunajipanga tuitumie kwetu ili tuinue sekta ya michezo kwa ujumla,” amesema Msigwa.

Msigwa amesema fedha wanazoingiza Japan kupitia bahati aasibu yao ni nyingi na wataiga jambo hilo kwa ajili ya maendeleo ya kichezo na sekta nzima kwa ujumla.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments