ARUSHA: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa huduma ya Internet bure (WiFi) katika kijiji cha Ngarash wilayani Monduli nyumbani kwa Hayati Edward Lowassa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Jabiri Bakari akizungumza amesema wamerahisisha shughuli ya mawasiliano kwa waombolezaji ili wasipate tabu katika kuwasiliana.
“Maeneo haya kumekuwa na watu wengi kwa gafla, tumeongea na watoa huduma wa mitandao ya simu wa ‘adjust’ huduma za mitambo yao ile lodi itakayokuwepo hapa itaweza kubebwa,”amesema Jabiri na kuongeza
“TTCL tayari imeshasogeza ‘fiber’ ili kupunguza lodi kwenye mitandao ikiwemo data, kutakuwa na free WiFi kwa waombolezaji.”amesema
Mwili wa Lowassa umeshawasili Monduli na maziko yanatarajiwa kuwa siku ya Jumamosi.
0 Comments