“Wananchi kachukueni vitambulisho vya Taifa”

MWANZA: KATIBU Tawala Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana amezindua ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa wananchi wa wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Balandya amewataka wananchi kufika kwenye vituo kujisajili na walivyojiandikisha kwenda wakachukue kadi zao kwani zipo tayari.

Balandya amebainisha kuwa tayari Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imekamilisha uzalishaji wa vitambulisho kwa wananchi wapatao 716, 245.

Amesema kwamba bado kuna vitambulisho vingi katika ofisi za Serikali za Mitaa na huku wananchi wakiwa na namba tu za kuwatambua jambo ambalo si sahihi hivyo ni wakati sasa wa kuvichukua kwa ajili ya rejea mbalimbali.

Balandya amesisitiza weledi na uzalendo kwa mamlaka kwenye utambuzi na usajili wa wananchi ili waandikishwe wenye sifa kwa mujibu wa sheria na si vinginevyo na kwamba kwenye utekelezaji wa zoezi hilo wasiliache kundi la watu wenye mahitaji maalum.

Ofisa usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Mwanza Daud Abdallah ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo kwani  kigezo kikubwa cha utambuzi na usajili ni kwa raia kuwa na miaka 18 na kwamba mamlaka hiyo imesajili asilimia 84 ya wenye sifa mkoani Mwanza na zoezi hilo ni endelevu.

‘’Kwa Mkoa wa Mwanza, mamlaka ilikuwa na lengo la kusajili wananchi 1,786,876 lakini mpaka sasa mamlaka imefanikiwa kusajili na kuwatambua wananchi na wageni wakazi kwa pamoja na idadi yao imefika 1,506,536 ambayo ni sawa na asilimia 84.3% ya malengo ya usajili kwa  Mkoa wa Mwanza’’ amesema.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments