Azam Yapata pointi 3 Dhidi Yanga kwa Mkapa

DAR ES SALAAM: MATAJIRI wa Chamazi, Azam FC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Yanga SC katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga wameanza mchezo huo kwa kupata bao la mapema, dakika 10′ mfungaji akiwa Clement Mzize na furaha kudumu kwa dakika tisa tu kabla ya mshambuliaji wa Gambia Gibril Sillah kusawazisha dakika ya 19′ na kuelekea mapumziko bila mbabe katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Dakika 51′ Feisal Salum Abdallah ‘Feitoto’ akawainua vitini wanazi wa Azam FC na kufanya dakika 90′ kutamatika kwa matajiri hao kuvuna alama tatu.

Matokeo haya yanaifanya Azam kupanda hadi nafasi ya pili wakiwa wamevuna alama 47 katika michezo 21 huku Yanga wakiendelea kushika usukani wa ligi kwa jumla ya alama 52

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments