Biteko ataka kasi usambazaji umeme vijiji 127 Shinyanga

KISHAPU, Shinyanga: VIJIJI 127 kati ya  509 mkoani Shinyanga bado havijapata umeme, hali iliyoifanya serikali kuwataka wakandarasi  ambao wamechelewa kufikia lengo la usambazaji umeme kwenye mkoa huo, kampuni ya Suma JKT na Tontan kuhakikisha kuwa wanamaliza kazi husika kwani uzembe kwenye miradi hiyo haukubaliki.

Akitoa maagizo hayo leo mkoani Shinyanga, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko ameziagiza TANESCO na REA kuhakikisha kuwa wanawapelekea wananchi umeme kwa haraka na kama kuna changamoto ya umeme wananchi hao wapate taarifa mapema.

Aidha Dk Biteko ameagiza Watendaji wa Serikali kuhakikisha kuwa wanaweka mitambo ya umeme Jua kwenye majengo yao ili kutokuwa tegemezi kwenye umeme wa gridi pekee na kusema kuwa Wizara ya Nishati na Taasisi zake zitaanza kutekeleza suala hilo.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments