BAADA ya kufunga bao moja dhidi ya Jwaneng Galaxy, Clatous Chama rasmi anamzidi Mbwana Samatta bao moja katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kabla ya mchezo wa leo, Chama alikuwa na mabao 21, sawa na Samatta na sasa anakuwa na mabao 22 na kushika nafasi ya nane katika orodha hiyo.
Chama amefunga mabao hayo akiwa RS Berkane na Simba SC.
Tresor Mputu, mshambuliaji wa zamani wa TP Mazembe anaongoza katika orodha hiyo akiwa na mabao 39.
Mohammed Aboutrika nyota wa zamani wa Al-Ahly anashika nafasi ya pili akiwa na mabao 31, wakati mchezaji wa zamani wa Al-Ahly Flavio Amado akiwa na mabao 30.
0 Comments