DAR ES SALAAM: Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umewataka wananchama wake kutumia vituo vya afya mbadala baada ya hospitali tano za Kairuki, TMJ, Apollo, Aga Khan na Regency kuvunja mkataba wa utoaji wa huduma baina yao na Mfuko.
Taarifa ya NHIF imesema Maofisa wake watakuwa katika vituo hivyo kuhakikisha wanachama wenye changamoto za tiba wanapata msaada katika vituo vingine.
Anjela Mziray, Meneja Uhusiano wa NHIF amesema leo Machi 1 kuwa Mfuko huo unaendelea kufanya usajili wa vituo vingine binafsi ili kuongeza wigo wa watoa huduma na kusogeza kuduma kwa wanachama.
0 Comments