SONGEA: Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala , Katiba na Sheria imeipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha katika miradi yenye tija Kwa watu kupitia mfuko wa TASAF.
–
Kamati imetoa pongezi hizo baada ya kukagua mradi wa Stendi ya Mabasi Peramiho na soko la bidhaa mbalimbali, Madaba.
–
Akizungumza mbele ya wananchi Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk Joseph Mhagama aliishukuru serikali kwa miradi hiyo .
–
Awali, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ridhiwani Kikwete alimshukuru Rais Samia kwa kuwezesha fedha kiasi cha Sh. Bilioni 1.5 kutekeleza miradi mbalimbali katika Mkoa wa Ruvuma pekee kupitia TASAF.
0 Comments