KAWAIDA AFUNGA MICHUANO YA SAMIA CUP JIMBO LA SAME MASHARIKI...

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Mohamed Ally Kawaida (MCC), amehitimisha mashindano ya mpira wa miguu ya Samia cup jimbo la Same mashiriki yaliyoshirikisha timu 91 ambayo yaliandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Anne Kilango Malecel.

Kawaida alisema kuwa, Mbunge Anne ameonyesha dhamira ya dhati ya kuiunua vipaji vya vijana kwa kuanzisha mashinado hayo ambayo yalichezwa kwa mfumo wa kitarafa na hatimaye mabingwa kukutanishwa ili kushindana kijimbo na kumpata bingwa wa Jimbo.

Alisema kuwa, michezo inasaidia vijana kutojiingiza katika mambo maovu kwa kuwafanya kuwa bize na michezo na kuwataka wabunge kuiga mfano huo alioanzisha Anne Kilango Malecel.

Kwa upande wake, Mbunge Anne aliwataka Vijana wa jimbo hilo kuanza maandalizi kwa ajili ya mashindano ya Hussein Mwingi cup yanayotarajiwa kuanza Novemba mwaka huu.

Mbunge huyo alisema kuwa, lengo la kuanzisha mashindano hayo yaliyokuwa akichezwa kwa Tarafa tatu na badae jimbo ni kuwakutanisha vijana pamoja na kuwaonyesha jinsi ambavyo serikali ya awamu ya sita inavyosamini michezo .

Kawaida alishuhudia fainali ya jimbo iliyozikutanisha timu kutoka kata ya Ndungu dhidi ya Kihurio ambapo Ndungu iliibuka mshindi kwa kuifunga Kihurio goli moja kwa bila.



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments