KIKWETE :Mapambano ya malaria yako karibu na moyo wangu

DAR ES SALAAM: RAIS Mstaafu wa Awamu ya nne, Dk Jakaya Mrisho Kikwete amesema suala la kupambana na malaria ni jambo ambalo liko karibu na moyo wake.

Aidha amempongeza na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa busara wa kuanzisha Baraza la Kutokomeza Malaria Tanzania ambapo ameutaja uamuzi huo kuwa ni muhimu,wenye tija na manufaa makubwa kwa nchi.

Aprili 25, 2023 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alizindua baraza hilo na kusema jukumu lake ni kukusanya rasilimali fedha kwaajili ya kupambana na ugonjwa huo kwa lengo la kufikia 0 malaria ifikapo 2030.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa tatu wa baraza hilo, Dk Kikwete amefafanua kuwa uamuzi huo umefanywa wakati muafaka kutokana na hali ya ugonjwa huo ilivyo duniani.
“Nampongeza Rais wetu mpendwa kwa kuwachagua ninyi kuwa wajumbe alivyopanga baraza ni jambo linastahili pongezi na ninathibitisha dhamira ya Rais kuona Tanzania inashinda dhidi ya malaria na kutokomeza.

“Ninakiri siku nilivyopata taarifa ya kuundwa na baraza hili nilijaa furaha tele kama Mtanzania na kama mjumbe mwasisi wa Baraza la Kutokomeza Malaria Duniani,ninafuraha kuwa mapambano ya malaria yanapewa msukumo stahiki hapa nchini,”alieleza Dk Kikwete.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments