Mafuriko yauwa 19 Indonesia

MVUA kubwa iliyosababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi katika kisiwa cha Sumatra nchini Indonesia, imeuwa takriban watu 19 na wengine saba kupotea, maofisa wamesema leo..

Tani za matope, mawe na miti iliyong’olewa ilibingirika chini ya mlima mwishoni mwa Ijumaa, na kufikia mto ambao ulipasua kingo zake na kusambaratisha vijiji vya milimani katika Wilaya ya Pesisir Selatan ya Mkoa wa Sumatra Magharibi, alisema Doni Yusrizal, ambaye anaongoza wakala wa kudhibiti majanga wa eneo hilo.

Waokoaji kufikia Jumamosi walitoa miili saba katika kijiji kilichoathirika zaidi cha Koto XI Tarusan, na kupata wengine watatu katika vijiji viwili vya jirani, Yusrizal alisema.

Waokoaji walipata miili sita katika Pesisir Selatan na wengine watatu katika Wilaya jirani ya Padang Pariaman, na kufanya idadi ya waliofariki kufikia 19, Shirika la Kitaifa la Kudhibiti Maafa limesema leo Jumapili.

Shirika hilo katika taarifa yake lilisema wanakijiji wawili walijeruhiwa na mafuriko hayo na waokoaji wanawasaka watu saba ambao inaripotiwa kuwa hawajapatikana.

Alisema zaidi ya watu 80,000 wamekimbilia kwenye makazi ya muda ya serikali baada ya mafuriko na maporomoko ya ardhi kubomoa nyumba 14, wakati nyumba 20,000 zimejaa maji katika wilaya na miji tisa katika Mkoa wa Sumatra Magharibi.

“Juhudi za kutoa misaada kwa waliofariki na waliopotea zilitatizwa na hitilafu za umeme, barabara zilizofungwa kwa matope na vifusi,” Yusrizal alisema.

Mvua kubwa husababisha maporomoko ya ardhi na mafuriko ya mara kwa mara nchini Indonesia, ambapo mamilioni ya watu wanaishi katika maeneo ya milimani au karibu na maeneo ya mafuriko.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments