MAJUMBA YA RAPA MAARUFU P. DIDDY YAVAMIWA NA MAWAKALA WA USALAMA WA NDANI WA NCHI MAREKANI KWA TUHUMA AMBAZO BADO KUTAJWA

Mawakala wa Usalama wa Nchi wa Marekani  (Homeland Security) jana Jumatatu walivamia jumba la Holmby Hills linalohusishwa na msanii maarufu wa rap Sean "Diddy" Combs au Puff Daddy au P. Diddy  na kampuni yake ya utayarishaji muziki na filamu.

Sababu hasa ya uvamizi huo bado kuwekwa  wazi lakini P. Diddy hivi karibuni amehusishwa na madai ya unyanyasaji wa kijinsia na biashara ya ngono.

Mawakala hao wa HSI walivamia Jumba katika mtaa wa 200 wa S. Mapleton Drive huko Holmby Hills, eneo la matajiri la Los Angeles linalojulikana kama mitaa ya watu mashuhuri na Jumba la Playboy.


Jumba hilo linahusishwa na kampuni ya utengenezaji wa Filamu za Bad Boy ya Combs.


Maajenti walionekana wakiwashikilia wanaume wawili ambao baadaye walitambuliwa kuwa ni watoto  wa Diddy, na kwamba 

Vijana  hao wawili hawakuwa wamekamatwa lakini walikuwa wakizuiliwa nje huku maajenti wakipekua Ndani ya jumba hilo.


"Mapema leo, Uchunguzi wa Usalama wa Nchi (HSI) New York ulichukua hatua za kutekeleza sheria kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea, kwa usaidizi kutoka kwa HSI Los Angeles, HSI Miami, na washirika wetu wa kutekeleza sheria katika eneo lako.


“Tutatoa taarifa zaidi kadri zitakavyopatikana," Idara hiyo ya Usalama wa Nchi ilisema katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari. Idara ya Sheriff ya Kaunti ya Los Angeles pia ilikuwepo katika kusaidia, idara hiyo ilithibitisha.


Wanawake ambao wametoa shutuma hadharani dhidi ya Diddy wameonesha kufurahishwa na uvamizi huo wa nyumba za P. Diddy.


Wakili Douglas Wigdor, anayemwakilisha Cassie Ventura na mlalamikaji ambaye jina lake lilijulikana kama Jane Doe, alitoa taarifa hii Jumatatu:


"Siku zote tutaunga mkono utekelezaji wa sheria unapotaka kuwafungulia mashtaka wale ambao wamekiuka sheria. Tunatumai huu ni mwanzo wa mchakato ambao

 itamshikilia Bw. Combs kuwajibika kwa mwenendo wake potovu."


Katika Mtandao wake wa X wenye wafuasi zaidi ya milioni 12, rapa mwingine maarufu, 50 Cents, amesema: “Hii ni dhahiri kwamba sio tena Diddy alifanya, ila nim Diddy kafanya. Hawa jamaa hawakuvamii hivi hivi kama huna kesi ya kujibu”. 


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments