Waziri Mkuu Mstaafu,MIZENGO PINDA, anatarajia kuwa mgeni rasmi kesho Ijumaa (Machi 15, 2024) katika mkutano mkubwa utakaowashirikisha wafugaji wa nyuki zaidi 800 kutoka wilaya zoye za Mkoa wa Singia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kijiji cha Nyuki Co. Ltd, Philemon Josephat Kiemi, akizungumza na waandishi wa habari leo (Machi 14,2024) amesema kauli mbili ya mkutano huo ni kuwawezesha wafugaji wadogo wa nyuki wa Mkoa wa Singida kuuza asali na bidhaa zitokanazo na nyuki nje ya nchi ambazo zimekidhi viwango vya kimataifa.
Amesema mkutano huu ambao utakuwa ni wa pili kufanyika kwa kuwa Februari 2015 ulishawahi kufanyika mwingine ambapo wafugaji wa nyuki wapatao 500 ambao walishiriki mafunzo ya jinsi ufugaji nyuki kibiashara watagawiwa mizinga ya nyuki,vazi la nyuki pamoja na kifaa cha kuvuna vumbi la Singida ambayo ni miongoni mwa bidhaa mpya inayozalishwa kutokana na nyuki.
Kiemi amesema pamoja na mambo mengine mkutano huo wafugaji wa nyuki wa Mkoa wa Singida watapitisha rasimu ya mwisho ya kuundwa kwa Umoja wa Wafugaji wa Nyuki Mkoa wa Singida ambao utakuwa na waanzilishi 800 kutoka katika kila kijiji na kata za mkoa hyu
Amesema kazi nyingine zitakazofanyika, mgeni rasmi Waziri Mkuu Mstaafu Pinda atazindua kitabu kitakachojulikana Ifoneo Singida Philemon Kiemi na Kijiji cha Nyuki.Kitabu hicho kitaelezea historia ya maisha ya Philemon Kiemi na kijiji cha Nyuki kwani watu wengi wamekuwa wakiuliza maswali kwamba kijiji hicho kilianzaje na kinafanya nini ambapo majibu yote yatapatikana kupitia kitabu hicho.
Chanzo Zaraafricablog
0 Comments