TANGA: Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi, Batilda Burian amewaapisha wakuu wa Wilaya ya Pangani na Lushoto leo na kuwataka kufanya kazi kwa uwadilifu weledi na utumishi katika kuwatumika wananchi katika nafasi zao walizopewa za kumuwakilisha Rais Samia.
Hayo ameyasema wakati wa hafla ya kuwaapisha wakuu hao wa wilaya katika ukumbi wa Halimashauri ya Wilaya ya Handeni ambapo amesema kuwa anategemea ubunifu katika utekelezaji wa majukumu yao sambamba na kutatua kero za wananchi.
“Nategemea nyie wakuu wa wilaya mtakua chachu ya maendeleo katika kukuza uchumi wa vipato vya wananchi kwenye maeneo yenu kwa kuibua fursa mbalimbali za kiuchumi hususani kilimo na viwanda”amesema RC Batilda.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Japhar kubecha amesema kuwa anakwenda kushirikiana na wananchi wa wilaya hiyo Kwa ajili ya kuwaletea maendeleo lakini na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo iweze kuwa ni yenye ubora.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mussa Kilakala amesema kuwa kutokana na Pangani kuwa kwenye ukanda wa Pwani anakwenda kutekeleza kwa vitendo sera ya uchumi wa bluu Ili iweze kuleta tija kwa wananchi sambamba na kuongeza mapato zaidi
0 Comments