TANTRADE YAPOKEA VIFAA VYENYE THAMANI YA BILIONI MOJA KUTOKA UBALOZI WA KOREA KUSINI

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade)  imepokea vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh.illioni Moja kutoka kwa ubalozi wa Korea Kusini.


Akizungumza katika hafla hiyo ya kupokea vifaa hivyo leo  machi 19, 2024 ,Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Latifa Khamis amevitaja vifaa walivyopokea ni  vibanda 500 vya kuoneshea maonesho, komputa mpakato 10, komputa za kawaida 30, scana 30 pamoja na jeneraita la KVT 60.

Amesema  vifaa hivyo ni muhimu na vya thamani kwa Mamlaka hiyo kwani vitaongeza mapato na kuleta ufanisi katika maonesho ya Biashara ya kimataifa (sabasaba)

Ameongeza  katika kuboresha zaidi maonesho ya kimataifa ya Biashara (sabasaba) Tanrade iliuomba ubalozi wa Korea kusini kupata vifaa ikiwemo vibanda  ambavyo vitasaidia katika kuboresha maonesho kwenda vizuri.

"Kama mnavyoshuhudia kila siku zinavyokwenda wadau wamekuwa wakiitaji kushiriki maonesho lakini wamekuwa wakikosa nafasi hivyo kupitia vibanda hivi tutaongeza washiriki na ufanisi pamoja na kuongeza mapato wa nchi."

Mbali na msaada huo pia  amesema wako katika mazungumzo baina ya Tan Trade na Ubalozi wa Korea Kusini yanayolenga zaidi kuboresha Utendaji kazi huku akifafanua mahusiano yao hayaishii Tan trade pake bali na katika maeneo mengine.


Aidha amesema  maonesho ya kimataifa ya Biashara ya 48 ya mwaka huu  yataimarika na yatakuwa  yenye mvuto zaidi.

Kwa upande wake Balozi wa Korea kusini, Kim Sun Pyo ameeleza kwamba wataendelea kushirikiana katika maeneo mbalimbali  huku akitoa rai kwa wafanyabiashara wa Tanzania kusafirisha bidhaa zao ili kwenda kuziuza Korea Kusini.

"Upo umuhimu wa kuwahamasisha wananchi wa Korea kusini  waweze kununua bidhaa kutoka Tanzania.Tunahitajika kuhamasisha uhusiano wa pande zote mbili katika masuala haya"ameongeza.TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments