TARURA MANISPAA YA SINGIDA KUTUMIA BIL.2.7/- KUTEKELEZA MIRADI YA BARABARA


Meneja wa TARURA Mkoa wa Singida Mhandisi IBRAHIM KIBASA amesema Halmashauri ya Manispaa ya Singida ina Bajeti ya Shilingi Bilioni 2.7 kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Barabara katika Manispa hiyo.

 

Mhandisi KIBASA alisema hayo mara baada ya kutembelea Barabara zinazojengwa kwa kiwango cha Lami na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijiji - TARURA katika Manispaa ya Singida.

 

Alisema hali ya utekelezaji wa Miradi ya Barabara katika Manispaa ya Singida imefikia asilimia 75 ya miradi yote ambayo inaendelea kutekelezwa.

 

Aidha alisema Halmashauri ya Manispaa ya Singida ina Mtandao wa Barabara wa Kilometa 523 na zote zipo katika mkakati wa kujengwa kwa kiwango cha Changarawe na Lami ili kuondoa changamoto ya ubovu wa Barabara.

 

KIBASA pia alitoa wito kwa wananchi kutunza miundombinu ya Barabara ili iweze kudumu kwa muda mrefu na iendelee kutoa huduma kwa wananchi.

 

Kwa upande wao Wananchi wa Manispaa ya Singida waliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN kupitia TARURA kwa kuendelea kujenga Barabara za la Lami katika maeneo yao na kuondoa changamoto ya usafiri iliyokuwa ikiwakabili hapo Awali.

 

Mmoja wa wananchi wa Manispaa ya Singida DEVOTHA CHARLES alisema awali changamoto ya barabara kabla hazijawekwa lami ilikuwa kubwa sana, hali inayosababisha washindwe kupata baadhi ya huduma za kijamii kama vile kwenda Hospitali.

 

Aidha alisema kwa sasa changamoto ya ubovu wa Barabara imeisha baada ya serikali kujenga Barabara za Lami ambazo kwa sasa wanapita bila usumbufu hasa kipindi cha Masika.

 

Naye SAID ATHUMAN ambaye ni Afisa Usafirishaji (Dereva Bajaji) alisema kwa sasa barabara zimekuwa nzuri hata vyombo vyao vya usafiri haviharibu mara kwa mara kutokana na ubovu wa Barabara.

 

Barabara zilizotembelewa na kukaguliwa na wahandisi wa TARURA ni Mwenge - Mungu Maji na Imbele - Mnung'una ambazo ujenzi wake upo hatua za mwisho kukamilika.


 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments