TFF Yakabidhi Mipira 1000 Shule Za Msingi Singida.


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limekabidhi mipira 1,000 kwa shule za msingi 50  Mkoani Singida, kwa lengo la kutekeleza programu za michezo shuleni.

Programu hiyo  ni football for school iliyoanzishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), ikiwa ni mbadala wa programu ya grassroot, ambapo lengo lake kuu ni kukuza vipaji kwa wanafunzi.

Akizungumza kwenye hafla  ya kukabidi mipira hiyo kwa niaba ya Rais wa TFF, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira miguu Mkoa huo (SIREFA)  Hamisi Kitila amesema Mkoa wa Singida umekuwa miongoni mwa mikoa bora inayoshiriki kwa ufanisi katika mchezo huo, Tanzania Bara na visiwani kwa ujumla.

Kitilla  ameeleza kuwa jumla ya shule 50  kwa mkoa huo zitapatiwa mipira hiyo, ambapo kila shule itapatiwa mipira 20, itakayotumiwa na wanafunzi katia mchezo wa mpira wa miguu.

“Ni matumaini ya Rais wetu wa TFF kuwa mipira hii inakwenda kufanya kazi iliyokusudiwa, tunataka kuona vipaji vinaibuliwa kupitia mipira hii, TFF na FIFA watakuwa wanakuja kufanya ukaguzi kuona kama mipira hii inaleta tija,” amesema Kitila

Aidha, Mwenyekiti huyo amemshukuru Rais wa TFF Wallace Karia kwa kutupatia Mkoa wa Singida kuwa miongoni mwa mikoa ya kupata mipira hiyo, ambao alieleza chama chake kitahakikisha vipaji vinaibuliwa kupitia vifaa hivyo.

Kabla ya zoezi la kugawa mipira hiyo kwa shule nufaika, Mkuu wa Mkoa  Singida huo  Piter Serukamba ameishukuru TFF, na kuagiza kila shule iliyopokea mipira hiyo, inahakikisha inatumika kwa watu sahihi.

Serukamba amesema kuwa michezo na elimu ni kitu kimoja.“ Sitegemei kuona au kusikia mipira hii inatumika kwa watu wazima, hii mipira imetolewa kwa wanafunzi wa shule za msingi, darasa la kwanza hadi saba...tunataka kuona Mkoa wa Singida unaendelea kutoa wanamichezo wa kitaifa na kimataifa.

Kwa Upande wa Mwenyekiti wa soka la wanawake  mkoa wa Singida na Meya wa Manispaa ya Singida Bi.Yagi Kiaratu ameeleza kuwa, mipira hiyo imekuja kwa wakati mwafaka, kutokana na shirikisho la mpira wa miguu duniani, FIFA na na hapa nchini TFF, yamedhamiria kuibua vipaji kuanzia ngazi za chini hadi taifa.

Bi. Yagi Kiaratu amesema kuwa “Kwa eneo hili, nina uhakika kupitia mipira hii, sasa tutakwenda kuibu vipaji halisi, ukosefu wa mipira ilikuwa ni changamoto kubwa, tunashukuru TFF na FIFA kwa kutatua changamoto hii,”amesema.

Na Abdul Bandola Singida.       

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments