POLISI wa Kiislamu wanaofahamika kwa jina la Hisbah Kaskazini mwa Jimbo la Kano nchini Nigeria wamewakamata waislamu 11 kwa kula mchana ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Msemaji wa Hisbah, Lawal Fagge aliripoti kukamatwa kwa wanaume 10 na mwanamke.
“Tulipokea watu 11 siku ya Jumanne akiwemo mwanamke aliyekuwa akiuza njugu ambaye alionekana akila kutoka bidhaa zake, na baadhi ya watu walituarifu,” Fagge alisema.
“Wengine 10 walikuwa wanaume na walikamatwa katika jiji lote hasa karibu na masoko ambapo shughuli nyingi hufanyika.”
Washtakiwa 11 baadaye walifutiwa makosa yao baada ya kuapa kutokula au kunywa. Zaidi ya hayo, familia zao ziliombwa kuhakikisha wanafunga.
0 Comments