WAZIRI BASHUNGWA AAGIZA WAHANDISI WASHAURI WANAOSHINDWA KUSIMAMIA MAKANDARASI WASIPEWE KAZI

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Wakala wa Barabara (TANROADS) kutowapatia kazi za usimamizi wa miradi Wahandisi Washauri wanaoshindwakuwasimamia Wakandarasi kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara kwa viwango namujibu wa mikataba na kupelekea Mkandarasi kurudishwa eneo la mradi kurudia kazi.

Bashungwa ameagiza hayo Machi 22, 2024 Wilayani Mafia wakati akikagua barabara ya Kilindoni - Utende (km 14.6) kwa kiwango cha lami, iliyojengwa na Mkandarasi CHICO na chini ya usimamizi wa Mhandisi Mshauri Kampuni ya UWP Tanzaniaambapo barabara hiyo haikutekelezwa kwa viwango na kusababisha Mkandarasikurudia sehemu ya kazi.

“Kama mlivyofanya katika mradi huu kwa kumrudisha Mkandarasi Site, WahandisiWashauri kama hawa wanaoshindwa kumsisimamia Mkandarasi wanapaswa wawe‘blacklisted’ kwa sababu tunawalipa pesa ya kumsimamia Mkandarasi kwaniaba ya Serikali”, amesema Bashungwa.

Bashungwa amemuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS kutompatia kazi yoyote ya kusimamia miradi Mhandisi Mshauri wa kampuni ya UWP Tanzania na wahandisi washauri wengine wa aina hiyo ambao wameshindwa kutekeleza wajibu wao kwakuwasimamia Makandarasi kutekeleza miradi kikamilifu na kuisababishia hasara Serikali.

“Mhandisi Mshauri UWP hafai na nikiona mmempa kazi sehemu yotote mimi na nyinyi na hii iwe funzo kwa Wahandisi Washauri wengine tunaowapa kazi ya kuwasimamia Makandarasi”, amesema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amesema kuwa Wizara ya Ujenzi itaendelea kuwasimamia Wakandarasi na Wahandisi Washauri walipatiwa kazi za kutekeleza miradi ili fedha zinazotolewa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ziweze kutekeleza na kukamilisha miradi kikamilifu kama ilivyokusudiwa.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Miradi kutoka TANROADS Eng. Malima Kusesa ameeleza kuwa ujenzi wa barabara ya Kilindoni - Utende (km 14.6) kwa kiwango cha lami ulikamilika mwaka 2015 na baada ya muda wa matazamio 2016 yalibainika mapungufu katika kipande cha kilometa nne.

Eng. Kusesa ameeleza kuwa baada ya kubainika mapungufu hayo, TANROADS walimtaka Mkandarasi CHICO na Mhandisi Mshauri UWP Tanzania kurudia kazi sehemu hiyo kwa gharama zao.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi


 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments