Kocha wa IHEFU Meck Meksime amesema wamejipanga kufanya vizuri katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB katika mchezo huo unaotarajiwa kupigwa katika uwanja wa CCM Liti Mkoani Singida, huku muwakilishi wa wachezaji Benjamen TANIM amesema wao kama wachezaji wamejianda vizuri kwenda kupambana na kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo.
Kwa upande wake kocha wa MASHUJA MOHAMED BARESI amesema itakuwa ni mechi ngumu lakini wao wamejianda vizuri kuhakikisha wanashinda mchezo huo ili waweze kusonga mbele kwani mshindi wa kombe hilo anaiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa.
ADAM ADAM amesema wao kama wachezaji wanamorali kubwa kufanya vizuri katika mchezo huo na kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo na IHEFU. |
ENDREW MHEZIWA, Meneja wa Biashara Kanda ya Kati CRDB amesema wao kama wadhamini wakuu wa Kombe la Shirikisho la CRDB, wanawatakia IHEFU na MASHUJA mchezo mzuri huku akisema mchezaji bora wa mcheza huo ataondoka na kitita cha shilingi Laki tano.
Mheziwa meneja wa biashara kanda ya kati CRDB ametoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuiamini benki ya CRDB na kuja kupata huduma mbalimbali za benki hiyo ikiwa ni pamoja na kufungua Akaunti.
0 Comments